UPIMAJI WA MALARIA KATIKA MADUKA YA DAWA MUHIMU

SAMSUNG CAMERA PICTURES
VITENDANISHI VINAVYOTUMIKA KATIKA UPIMAJI WA MALARIA

Hali ya Malaria nchini imepungua katika kipindi cha muongo (Miaka kumi) mmoja baada ya kutekeleza afua za kudhibiti malaria pamoja na kutumia njia nyingine za afya. Maambukizi ya malaria yamepungua kutoka asilimia 18% mwaka 2007/8 hadi kufikia 9.5% mwaka 2011/12. Sambamba na hali hiyo, mpango mkakati wa kudhibiti malaria kwa mwaka 2014 – 2020 ni kutimiza lengo la kupunguza maambukizi ya malaria kutoka wastani wa asilimia 10% kitaifa mwaka 2012 hadi kufikia kiwango cha asilimia 5% mwaka 2016 na hatimaye chini ya asilimia 1% ifikapo mwaka 2020.

Read more…

VITAMBUE VIPODOZI VYENYE VIAMBATA HATARISHI

vipodozi hatarishi
MATUMIZI YA VIPODOZI

Vipodozi ni vitu ambavyo siku zote katika maisha yetu ya kila siku tumekuwa tukivitumia ili kuiweka miili yetu katika hali ya usafi, lakini pia vimekuwa vikichangia katika utanashati wa mtu.

Mpenzi msomaji, mara nyingi kwa baadhi ya watu wanaposikia neno kipodozi basi mawazo yao huamia katika vitu ambavyo hudhani hutumika kwa wanadada/wanawake peke yao, au hudhani kipodozi ni kile kitu kinachoweza kuchubua ngozi ya mtu na kumfanya aonekane na rangi ya ngozi nyeupe badala ya ile ya asili yake mfano nyeusi. Kipodozi ni pamoja na sabuni tunazotumia kila siku, mafuta ya kujipakaa, losheni, pafyumu,  krimu na jeli ambavyo hutumiwa na watu wa jinsia zote. Maana ya kipodozi haitabadilika ingawa vitu hivi vipo vya wanawake na pia wanaume. vyote huitwa vipodozi.

Read more…

MAMBO YA KUKUMBUKA KABLA YA KUTUMIA DAWA

TUMIA DAWA INAPOHITAJIKA
TUMIA DAWA INAPOHITAJIKA

Mpenzi msomaji, ni siku nyingine tena ambayo kwa mapenzi ya mwenyezi Mungu tumeweza kuiona na hatuna budi kumshukuru Mungu kwa wema wake.

Napenda kuchukua nafasi hii kukuarika wewe ndugu msomaji, ili tuweze kwenda pamoja katika kujifunza na kujikumbusha mambo muhimu mbalimbali yahusuyo afya zetu, mambo muhimu kabisa kuhusu dawa na matumizi yake kwa ujumla.

Katika somo letu la leo tutajifunza au kujikumbushia mambo makuu matatu, mambo hayo ni maana halisi ya dawa, wakati ambao mtu anahitajika kutumia dawa na pia tutajifunza/kujikumbusha kuhusu matumizi salama ya dawa.

Read more…